Ujasiriamali Consultancy over the world

UFUGAJI WA KUKU WENYE TIJA

(Kuku watano wa kienyeji upate kuku 200 kwa miezi 6)

HISTORIA NA MAANA YA KUKU

Kuku yupo katika kundi la ndege wanaofugwa na binadamu, katika kundi hili la ndege pia kuna bata mzinga, njiwa kanga na kadhalika. Njiwa, bata na bata mzinga walianza kufugwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita huko China. Kuku nao yasemekana yamkini walianza kufugwa miaka hiyo hiyo walipotolewa kwenye misitu ya ndege ya ki-Asia. Baadae ndege walianza kufugwa maeneo mbalimbali ya Bara la Ulaya na Marekani, walifugwa kwa njia ya kienyeji. Mnamo karne ya 16 waliingia Marekani wakitokea Ulaya na bata Mzinga waliingia Ulaya wakitokea Marekani. Njia za kisasa za uanguaji wa mayai ulianza mnamo miaka ya 1870 lakini si kwa ajili ya biashara huko China na Misri zama hizo. Ufugaji wa ndege kwa njia ya kisasa ulianza mbalimbali za ujengaji wa nyumba, ulishaji WA ndege na uzalishaji WA kuku ziliibuliwa na zilipelekea kukua kwa kasi uzalishaji WA ndege hasa kuanzia miaka ya 1930. Lakini ufugaji huu na ulaji uliongezeka zaidi kipindi cha vita kuu ya dunia kulipotokea uhaba wa nyama ya ng'ombe na nguruwe.

VYAKULA CHA KUKU

(1) Unga wa nafaka/dona kama mahindi au mtama.
(2) Pumba za mtama au pumba za mahindi au uwele.
(3) Mashudu ya Alizeti au ufuta au pamba au karanga n.k 17 kg.
(4) Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25
(5) Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10
(6) Chumvi 0.5 kg

VYAKULA VYA KUKU TYPE 2: In Percentage

Paraza soya 2.80 kg, dagaa 5.40 kg, Mashudu 4.40 kg, chokaa 4.02 kg, Crude protein 13.30

NJIA TOFAUTI ZA KULEA NA KUFUGA KUKU

(1) NJIA HURIA
Kuku huachwa wajitafutie chakula na maji  wenyewe. Njia hii hutumika sana kwa kuku wa kienyeji, ni mara chache sana mfugaji huwapatia chakula cha ziada. Kwa ufugaji wa namna hii ni lazima uwe na eneo kubwa la kutosha.

FAIDA
(1) Ni njia rahisi ya kufuga
(2) Gharama yake ni ndogo
(3) Kuku wanapata mazoezi ya kutosha
(4) Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya

HASARA
(1) Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na WANYAMA wakali na hali mbaya ya hewa
(2) Ukuaji wa kuku ni hafifu sana kufikia kilo 1.2 ni baada ya mwaka mmoja
(3) Huharibu mimea kama vile kula mimea na mazao ya bustani.
(4) Ni rahisi kuambukizwa magonjwa

(2) KUFUGA NUSU BANDA NDANI NA NUSU BANDA NJE
Huu ni mfumo wa  ufugaji ambao kuku wanakuwa na banda lililo - unganishwa uzio kwa upande wa mbele. Hapo kuku wanaweza kushinda ndani au nje ya banda lililo - zungushiwa uzio.

FAIDA
(1) Kuku wanakuwa salama na maadui mbalimbali
(2) Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri, hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama. Pia kuku hukua haraka
(3) Itakuwa rahisi kudhibiti wadudu navimelea vinavyoweza kuleta magonjwa.
(4) Ni rahisi kuwatenganisha kuku wako na kuwahudumia ipasavyo
(5) Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa
(6) Kuku hawaharibu mazao ya shambani wala bustani
(7) Utapata urahisi wa kupeleka mbolea shambani.

HASARA/CHANGAMOTO
(1) Uwe na muda wa kutosha kuwahudumia
(2) Uwe na eneo kubwa la kuwafugia
(3) Gharama kubwa ya kuandaa banda
(4) Hata hivyo, gharama hiyo huzidiwa na mapato utakayokuja kuyapata

(3) KUFUGA NDANI YA BANDA TU
Katika njia hii kuku hukaa ndani muda wote. Njia hii hutumiwa zaidi na kuku wa kisasa lakini huweza kutumiwa na kuku wa kienyeji pia. Hasa sehemu ambazo kuna uhaba wa maeneo.

CHANGAMOTO
(1) Unatakiwa uwe na muda wa kutosha kuwahudumia kuku kikamilifu.
(2) Unatakiwa uwe na mtaji mkubwa wa chakula na ujenzi wa mabanda.
Ugonjwa ukiingia ni rahisi kuambukizana. Pia wanaweza kuanza tabia mbaya ya kudonoana.


Comments