Ujasiriamali Consultancy over the world
UFUGAJI WA KUKU WENYE TIJA (Kuku watano wa kienyeji upate kuku 200 kwa miezi 6) HISTORIA NA MAANA YA KUKU Kuku yupo katika kundi la ndege wanaofugwa na binadamu, katika kundi hili la ndege pia kuna bata mzinga, njiwa kanga na kadhalika. Njiwa, bata na bata mzinga walianza kufugwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita huko China. Kuku nao yasemekana yamkini walianza kufugwa miaka hiyo hiyo walipotolewa kwenye misitu ya ndege ya ki-Asia. Baadae ndege walianza kufugwa maeneo mbalimbali ya Bara la Ulaya na Marekani, walifugwa kwa njia ya kienyeji. Mnamo karne ya 16 waliingia Marekani wakitokea Ulaya na bata Mzinga waliingia Ulaya wakitokea Marekani. Njia za kisasa za uanguaji wa mayai ulianza mnamo miaka ya 1870 lakini si kwa ajili ya biashara huko China na Misri zama hizo. Ufugaji wa ndege kwa njia ya kisasa ulianza mbalimbali za ujengaji wa nyumba, ulishaji WA ndege na uzalishaji WA kuku ziliibuliwa na zilipelekea kukua kwa kasi uzalishaji WA ndege hasa kuanzia miaka ya 1930. Lakini ufuga...